Leo tutaangalia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa
kutumia njia rahisi. Na jinsi gani unaweza kuzalisha kuku chotara. Kuku chotara
ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kabla hatujangalia hatua muhimu
za kuzalisha kuku chotara, tutaangalia faida za kuku chotara kwa
mwekezaji/mjasiriamali.
Faida za kuku chotara
kwa mfugaji na mlaji
Ukuaji mzuri
Nyama yake ina ladha nzuri na laini
Nyama yake ina ladha nzuri na laini
n.k
HATUA
MUHIMU KATIKA UZALISHAJI WA KUKU CHOTARA
Hatua
ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku,
banda la kuku linatakiwa liwe lina
pitisha hewa ya kutosha na kama unataka kufahamu kwa undani kuhusu maandalizi muhimu
ya banda lako. Makala hiyo itakuja kupitia blog yako ya uwekezaji na mtanzania.
Hatua
ya pil,i andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya
kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na
jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa
kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea
kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.
Hatua
ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako,
unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako
ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.
Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari
kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa
ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo
muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa
wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.
Chanjo
na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa
Siku 2-6 Pullorum
Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji
Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji

KUMBUKA
Dawa
ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatuImeandikwa: Emmanuel Mahundi
Kutoka wekezamtanzania.blogspot.com
No comments:
Post a Comment