1. Mafua ya kuku (Fowl
coryza)
Mafua kwa kuku mara nyingi husababisha na bacteria, ila mara zote chanzo
kikubwa cha ugonjwa huu ni kutokuwa na usafi mzuri wa banda la kuku.
Dalili za ugonjwa
huu: kuku kuhema kwa shida, kukoroma, kutiririsha kamasi puani, utelezi wa
kamasi mdomoni na kuku kuvaa koti. Ili kuweza kutambua dalili za ugonjwa mapema
ni vizuri ukiwa unawapa chakula kuku kuwaangalia kwa a makini.
Matibabu: Usafi wa banda, kuwatenga kuku ambao wanahumwa, kuchanja
kuku na kuwapa antibiotic kama OTC 20%, OTC 50%, sulphamethazine, streptomycine na vitamin. Dawa nyingine
vitunguu swaumu robo vimenye, twanga, changanya maji lita moja, chuja na uwape
kuku kwa wiki moja vile vile husaidia kutibu homa ya matumbo
2. Ndui ya
kuku (Fowl pox)
Kuku hupatwa na malenge kwenye kishungi na sehemu
zisizo na manyoya, vile vile kuku kuvimba macho na kuwa na usaha.
Matibabu: kuku wachanje wakiwa na umri
wa miezi miwili na wale ambao wameambukizwa watengwe na kupatiwa salfa.
Mara nyingi ugonjwa huu unasababishwa na vyombo
kutokuwa safi na kuku kupata choo cheupe.
Dalili za
ugonjwa:
kuku kuharisha nyeupe, kuku kupoteza hamu ya kula, kuku kusinzia, na kuku kuvaa
makoti.
Matibabu: usafi wa vyombo,
usafi wa banda, watenge kuku wagonjwa na kuwapatia dawa Amporium, Typhoprim Furazolidone
au Sulfadimidine.
Kwa maelezo zaidi/ushauri tuma ujumbe mfupi kwa
emmanuelmahundi@gmail.com