Ufugaji wa kuku kuna changamoto kubwa ya kuku kupata
magonjwa ambayo yataathiri ukuaji wake au kuku kufa. Magonjwa mengi kuku
huyapata kutokana na banda kutokuwa safi, kuingia kwa ugonjwa katika banda,
kutofuata taratibua za kinga na magonjwa ya mlipuko.
Haya ni kati magonjwa
ambayo kuku huyapata katika vipindi tofauti vya ukuaji wake
Kuharisha damu
Dalili ya kuku kuharisha damu kama vile kuku kupata kinyesi
cha damu, kuku kushuka mabawa na kuku kutochangamka.
Kutibu; usafi wa
banda la kuku, kuwatenga kuku wenye homa na vile vile tumia dawa ya amporium,
Typhoprim, Esb3 n.k
Kideri (Newcastle)
Husababishwa
na virusi na dalili zake kama kuku kupumua kwa shida, kuku kuhara na kuku hufa
wengi kwa mkupuo.
Kutibu; kuku wachanjwe katika
juma la kwanza, baada ya wiki mbili, baada ya kufikisha miezi mine na kila
baada ya miezi miwili au mitatu.
Endelea
kutembelea mtandao huu kujifunza magonjwa zaidi ambayo kuku huyapata.
Nakutakia mafanikioa mema katika maisha yako mwaka 2015
Kwa maelezo zaidi/ushauri tuma ujumbe mfupi kwa
No comments:
Post a Comment