Biashara ya ufugaji inahitaji maandali kama zilivo
biashara zingine. Ufugaji wa kuku unahitaji maandali ya msingi ili uweze
kufanya kwa ufanisi na ubora. Maandalizi yanamuhusu mfugaji kujifunza vitu
vingi ambavyo vinahusiana na ufugaji wa kuku.
Hivi ni vitu vya msingi kuvifahamu kabla ujaingia
katika ufugaji
Jifunze
kuhusu ufugaji wa kuku
Katika kujifunza huku, tafuta watu ambao
wanajishughulisha na ufugaji wa kuku kulinga na aina ya kuku ambao unahitaji
kufuga au kupitia semina na mtandao kama huu. Katika kujifunza zingatia vitu
vya msingi kama vile aina ya kuku, ukubwa wa banda, magonjwa na soko la kuku.
Ukubwa
wa banda pamoja na idadi ya kuku
Kama mjasiriamali ambaye umehamua kuingia katika
biashara ni vizuri ukatafuta watu wazoefu au wataalamu kujua ni aina gani ya
banda linafaa katika mazingira yako. Vile vile kufahamu ukubwa wa banda na
idadi ya kuku, ili usije ukajenga banda ambalo haliendani na idadi ya kuku na
kusababisha kuku kukua kwa shida na kuambukizana magonjwa.
Aina
ya kuku
Vile vile kama mfugaji anatakiwa kuwa makini katika
kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga. Aina ya kuku ina mchango mkubwa katika
biashara hii. Kuku wengine hushambuliwa sana na magonjwa, hawatagi vizuri au
ukuajia wake ni wa taratibu. Kwa kama mfugaji lazima uwe na taarifa ya aina ya
kuku ambao ni bora.
Kuhusu
chakula cha kuku
Ili kuku wakue vizuri wanahitaji mchanganyiko ya
chakula ambacho kinakizi mahitaji yao. Kwa hiyo ni vema kwa mfugaji kuwa na fomula
ya uchanganyaji wa chakula au kununua chakula ambacho ni bora. Kwa sababu
ukuajia wa kuku unategemea asilimia kubwa kutoka katika chakula wanachokula.
Usafi
wa banda
Sehemu kubwa ya magonjwa ya kuku yanatokana na banda
kutokuwa usafi ukiachilia magonjwa ya milipuko. Kwa ni vizuri kuhakikisha kuwa
banda la kuku linakuwa safi pamoja na vyombo vya chakula pamoja na maji. Vitu
hivi visipokuwa safi mara nyingi huchangia kuku kupata magonjwa.
Magonjwa
yanayowasumbua kuku
Mfugaji ni vizuri ukawa na taarifa na kujifunza
kuhusu magonjwa ambayo huwashambulia kuku. Ni vizuri ukajifunza dalili zake na
tiba ya magonjwa mbalimbali na jinsi ya kuyazuia. Vile vile ukajifunza katika
kuwapa kuku chanjo zao katika muda muafaka.
Ukajifunza
jinsi kupata masoko
Kama mjasiriamali ni vizuri ukajifunza mapema kuhusu
jinsi ya kupata masoko ya bidhaa zako kama vile mayai na kuku. Upatikana wa
soko ndio kitu kitakochafanya biashara yako izidi kustawi na kukua. Unatakiwa
kufahamu soko la bidhaa yako mapema ili kuwa na uhakika na biashara yako.
Haya yote
utajifunza wapi?
Sehemu kubwa ya kupata maarifa haya tembelea mtandao
huu kila siku na upate kujifunza mambo mengi kuhusu ufugaji wa kuku.
No comments:
Post a Comment