Monday, 16 February 2015

HII NDIO NJIA RAHISI AMBAYO UNAWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA

Leo tutaangalia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa kutumia njia rahisi. Na jinsi gani unaweza kuzalisha kuku chotara. Kuku chotara ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kabla hatujangalia hatua muhimu za kuzalisha kuku chotara, tutaangalia faida za kuku chotara kwa mwekezaji/mjasiriamali.

Faida za kuku chotara kwa mfugaji na mlaji
Ukuaji mzuri
Nyama  yake ina ladha nzuri na laini
n.k









HATUA MUHIMU KATIKA UZALISHAJI WA KUKU CHOTARA

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe  lina pitisha hewa ya kutosha na kama unataka kufahamu kwa undani kuhusu maandalizi muhimu ya banda lako. Makala hiyo itakuja kupitia blog yako ya uwekezaji na mtanzania.

Hatua ya pil,i andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.

Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa
Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji
Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji
KUMBUKA
Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu


Imeandikwa: Emmanuel Mahundi
Kutoka wekezamtanzania.blogspot.com

Wednesday, 28 January 2015

HAYA NI KATI MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA KUKU



1. Mafua ya kuku (Fowl coryza)
Mafua kwa kuku mara nyingi husababisha na bacteria, ila mara zote chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni kutokuwa na usafi mzuri wa banda la kuku.












Dalili za ugonjwa huu: kuku kuhema kwa shida, kukoroma, kutiririsha kamasi puani, utelezi wa kamasi mdomoni na kuku kuvaa koti. Ili kuweza kutambua dalili za ugonjwa mapema ni vizuri ukiwa unawapa chakula kuku kuwaangalia kwa a makini.

Matibabu: Usafi wa banda, kuwatenga kuku ambao wanahumwa, kuchanja kuku na kuwapa antibiotic kama OTC 20%, OTC 50%, sulphamethazine, streptomycine na vitamin. Dawa nyingine vitunguu swaumu robo vimenye, twanga, changanya maji lita moja, chuja na uwape kuku kwa wiki moja vile vile husaidia kutibu homa ya matumbo

2. Ndui ya kuku (Fowl pox)
Kuku hupatwa na malenge kwenye kishungi na sehemu zisizo na manyoya, vile vile kuku kuvimba macho na kuwa na usaha.







Matibabu: kuku wachanje wakiwa na umri wa miezi miwili na wale ambao wameambukizwa watengwe na kupatiwa salfa.

3. Kuharisha nyeupe (homa ya matumbo)
Mara nyingi ugonjwa huu unasababishwa na vyombo kutokuwa safi na kuku kupata choo cheupe.

Dalili za ugonjwa: kuku kuharisha nyeupe, kuku kupoteza hamu ya kula, kuku kusinzia, na kuku kuvaa makoti.

Matibabu: usafi wa vyombo, usafi wa banda, watenge kuku wagonjwa na kuwapatia dawa Amporium, Typhoprim Furazolidone au Sulfadimidine.

Kwa maelezo zaidi/ushauri tuma ujumbe mfupi kwa
emmanuelmahundi@gmail.com

Thursday, 22 January 2015

Mambo ya msingi kuyafahamu kabla ujaanza ufugaji wa kuku



Biashara ya ufugaji inahitaji maandali kama zilivo biashara zingine. Ufugaji wa kuku unahitaji maandali ya msingi ili uweze kufanya kwa ufanisi na ubora. Maandalizi yanamuhusu mfugaji kujifunza vitu vingi ambavyo vinahusiana na ufugaji wa kuku.












Hivi ni vitu vya msingi kuvifahamu kabla ujaingia katika ufugaji

Jifunze kuhusu ufugaji wa kuku
Katika kujifunza huku, tafuta watu ambao wanajishughulisha na ufugaji wa kuku kulinga na aina ya kuku ambao unahitaji kufuga au kupitia semina na mtandao kama huu. Katika kujifunza zingatia vitu vya msingi kama vile aina ya kuku, ukubwa wa banda, magonjwa na soko la kuku.

Ukubwa wa banda pamoja na idadi ya kuku
Kama mjasiriamali ambaye umehamua kuingia katika biashara ni vizuri ukatafuta watu wazoefu au wataalamu kujua ni aina gani ya banda linafaa katika mazingira yako. Vile vile kufahamu ukubwa wa banda na idadi ya kuku, ili usije ukajenga banda ambalo haliendani na idadi ya kuku na kusababisha kuku kukua kwa shida na kuambukizana magonjwa.

Aina ya kuku
Vile vile kama mfugaji anatakiwa kuwa makini katika kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga. Aina ya kuku ina mchango mkubwa katika biashara hii. Kuku wengine hushambuliwa sana na magonjwa, hawatagi vizuri au ukuajia wake ni wa taratibu. Kwa kama mfugaji lazima uwe na taarifa ya aina ya kuku ambao ni bora.

Kuhusu chakula cha kuku
Ili kuku wakue vizuri wanahitaji mchanganyiko ya chakula ambacho kinakizi mahitaji yao. Kwa hiyo ni vema kwa mfugaji kuwa na fomula ya uchanganyaji wa chakula au kununua chakula ambacho ni bora. Kwa sababu ukuajia wa kuku unategemea asilimia kubwa kutoka katika chakula wanachokula.

Usafi wa banda
Sehemu kubwa ya magonjwa ya kuku yanatokana na banda kutokuwa usafi ukiachilia magonjwa ya milipuko. Kwa ni vizuri kuhakikisha kuwa banda la kuku linakuwa safi pamoja na vyombo vya chakula pamoja na maji. Vitu hivi visipokuwa safi mara nyingi huchangia kuku kupata magonjwa.

Magonjwa yanayowasumbua kuku
Mfugaji ni vizuri ukawa na taarifa na kujifunza kuhusu magonjwa ambayo huwashambulia kuku. Ni vizuri ukajifunza dalili zake na tiba ya magonjwa mbalimbali na jinsi ya kuyazuia. Vile vile ukajifunza katika kuwapa kuku chanjo zao katika muda muafaka.

Ukajifunza jinsi kupata masoko
Kama mjasiriamali ni vizuri ukajifunza mapema kuhusu jinsi ya kupata masoko ya bidhaa zako kama vile mayai na kuku. Upatikana wa soko ndio kitu kitakochafanya biashara yako izidi kustawi na kukua. Unatakiwa kufahamu soko la bidhaa yako mapema ili kuwa na uhakika na biashara yako.

Haya yote utajifunza wapi?
Sehemu kubwa ya kupata maarifa haya tembelea mtandao huu kila siku na upate kujifunza mambo mengi kuhusu ufugaji wa kuku.



Wednesday, 21 January 2015

Haya ndio magonjwa ambayo kuku huyapata



Ufugaji wa kuku kuna changamoto kubwa ya kuku kupata magonjwa ambayo yataathiri ukuaji wake au kuku kufa. Magonjwa mengi kuku huyapata kutokana na banda kutokuwa safi, kuingia kwa ugonjwa katika banda, kutofuata taratibua za kinga na magonjwa ya mlipuko.













Haya ni kati magonjwa ambayo kuku huyapata katika vipindi tofauti vya ukuaji wake

Kuharisha damu
Dalili ya kuku kuharisha damu kama vile kuku kupata kinyesi cha damu, kuku kushuka mabawa na kuku kutochangamka.
Kutibu; usafi wa banda la kuku, kuwatenga kuku wenye homa na vile vile tumia dawa ya amporium, Typhoprim, Esb3 n.k

Kideri (Newcastle)
Husababishwa na virusi na dalili zake kama kuku kupumua kwa shida, kuku kuhara na kuku hufa wengi kwa mkupuo.
Kutibu; kuku wachanjwe katika juma la kwanza, baada ya wiki mbili, baada ya kufikisha miezi mine na kila baada ya miezi miwili au mitatu.

Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza magonjwa zaidi ambayo kuku huyapata.

Nakutakia mafanikioa mema katika maisha yako mwaka 2015

Kwa maelezo zaidi/ushauri tuma ujumbe mfupi kwa

Njia tofauti za kufuga kuku wa kienyeji



Kuku ni jamii ya ndege ambao hufuga katika mazingira kawaida ambayo binadamu wanaishi. Kuna aina nyingi za kuku a) kuku wa kienyeji b) kuku wa kisasa. Katika ufugaji wa kuku kuana aina tofauti za ufugaji wa kuku ambazo hutumika. 

Katika somo la leo tutaangalia ufugaji wa kuku wa kienyeji katika mazingira ya kawaida.
Katika kuchagua aina ya ufugaji wa kuku hutokana na mahitaji husika na gharama za kutengeneza banda pamoja na chakula.

Hizi ndio njia 3 unazoweza kutumia kufuga kuku katika mazingira ya kawaida

Ufugaji wa kuku huria
Katika ufugaji huu kuku hujitafutia chakula wao wenyewe. Ufugaji wa kuku huria unahitaji kuwa na eneo kubwa ambalo kuku wataweza kujitafutia chakula chao wao wenyewe. Ufugaji wa kuku huria hauna gharama kubwa za uendeshaji na kuku hulala eneo ambalo sio rasmi. Faida za ufugaji wa kuku huria; unahitaji gharama ndogo, ni njia rahisi na kuku wanapata mazoezi ya kutosha.

Hasara za kufuga kuku huria ni rahisi kupata magonjwa, ukuaji wa kuku ni mdogo na kuna hatari ya kupata magonjwa.
ufugaji wa kuku huria












Ufugaji wa kuku nusu huria (nusu ndani – nusu nje)
Katika ufugaji huu kuku wanakuwa wanaishi nje ambapo panauwa pamezungushiwa uzio na kuna kuwa na banda ambalo hutumia kutagia, kuatamia na kulala. Katika ufugaji inakuwa rahisi kuwa chakula, kudhibiti magonjwa, utaepusha uwezekano wa kuku kuibiwa na kuweza kuwatambua kuku wagonjwa.

Changamoto ya kufuga kuku nusu huria unahitaji gharama kubwa, unahitaji eneo kubwa na unahitaji muda mwingi kuwepo ili kuwangalia na kuwapa chakula.
ufugaji wa kuku nusu huria











Ufugaji wa kuku ndani ya banda
Ni ufugaji ambao kuku wanaishi katika banda kwa muda wote bila kutoka nje. Katika ufugaji kuku wanahitaji kupewa chakula bila ya wao wenyewe kujitafutia. Katika ufugaji unahitaji kuandaa banda bora kuku. Faida ya ufugaji wa kuku ndania ya banda kama ni rahisi kudhubiti maonjwa na upotevu wa mayai, vile vile ni rahsi katika kuwapatia chakula kulingana na makundi ya kuku.

Changamoto za ufugaji huu ni gharama kubwa kuandaa banda na kuwapatia chakula, ni rahisi ugonjwa ukiingia kuambukizana kuku wote. 
ufugaji wa kuku ndani ya banda













Nakutakia mafanikioa mema katika maisha yako mwaka 2015
Kwa maelezo zaidi/ushauri tuma ujumbe mfupi kwa
emmanuelmahundi@gmail.com